Jumatano, 22 Mei 2013

KATIBU MKUU MALIASILI NA UTALII ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA MKOMAZI

Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi alianza 
ziara yake Same kwa kufika ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya 
Same Mwalimu Herman Kapufi kujitambulisha.
Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi na ujumbe 
wake wakipitia baadhi ya kurasa katika kitabu hicho.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Donat Mnyagatwa
(aliyenyoosha mkono) akimuonyesha Katibu Mkuu 
Bi. Maimuna Tarishi (suti nyeusi) eneo lenye mgogoro wa 
mpaka katika Hifadhi ya Mkomazi. Wengine pichani kutoka
 kulia ni Mkurugenzi wa Malikale Donatius Kamambaa; 
Kaimu Mkurugenzi wa Mipango wa TANAPA 
Dk. Ezekiel Dembe na Mkurugenzi wa 
Utumishi Wizara ya Maliasili na Utalii Said Msambachi.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Donat Mnyagatwa 
akitoa Taarifa ya Hifadhi ya Mkomazi kwa Katibu Mkuu 
Maliasili na Utalii pamoja na ujumbe wake.
Watumishi wa Hifadhi ya Taifa Mkomazi wakiwa makini
 kumsikiliza Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna 
Tarishi alipowatembelea.
Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi 
(wa pili kulia) akizungumza na watumishi wa
 Hifadhi ya Mkomazi. Wengine pichani kutoka kulia ni 
Mkurugenzi wa Malikale Donatius Kamamba, 
Mkuu wa Hifadhi ya Mkomazi Donat Mnyagatwa na
 Mkurugenzi wa Utumishi wa Wizara ya Maliasili na 
Utalii Said Msambachi.
Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi katika 
picha ya pamoja na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.
Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi akiangalia 
mbwa mwitu waliohifadhiwa katika uzio maalum kwa ajili ya
 kuwalinda Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.
Picha zote na Pascal Shelutete.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni